Gossip

ZUCHU AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BOSI WAKE DIAMOND PLATINUMZ

ZUCHU AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BOSI WAKE DIAMOND PLATINUMZ

Msanii wa Bongofleva Zuchu amekanusha fununu za kuwa amevalishwa pete ya uchumba na Familia ya Diamond Platnumz imepeleka barua ya uchumba kwenye familia yake.

Akipiga na Wasafi FM  Zuchu pia Amekanusha madai ya kuishi nyumba moja na Boss wake Diamond Platnumz kwa kusema kuwa kila mtu anaishi nyumbani kwake.

Sanjari na hilo amethibitisha kuwa yupo kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hajamtaja jina lakini amemtaja kwa mwonekano kwa kusema kwamba ni mrefu ,ana rangi ya maji ya kunde,ni mfanya mazoezi,na mfanyabiashara.

Sifa ambazo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamejaribu kuziunganisha na mwonekano wa Diamond Platnumz ambaye  amekuwa akifanya sana mazoezi siku za hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *