Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu, amevunja ukimya wake kufuatia taarifa za ghasia zilizoibuka nchini Tanzania baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, ambazo zimeripotiwa kusababisha vifo vya baadhi ya wananchi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu ameomba Mungu aihifadhi Tanzania na kuijaalie amani, umoja na upendo, akionekana kuguswa na machafuko yanayoripotiwa katika baadhi ya maeneo nchini humo wakati wa uchaguzi.
Kauli ya Zuchu inakuja wakati ambapo mashabiki na wananchi kadhaa wamekuwa wakiwakosoa mastaa wa Tanzania kwa kile kinachoonekana kama ukimya wao kuhusu matukio ya ukatili na ghasia zilizoripotiwa kufuatia uchaguzi huo.
Hadi sasa, mamlaka husika bado hazijatoa takwimu rasmi za watu walioumia au kupoteza maisha katika vurugu hizo, huku viongozi wa dini na wasanii wengine wakihimiza mazungumzo na utulivu nchini.