Entertainment

Zuchu Asema Hatima ya Ndoa Yake na Diamond Ipo Mikononi mwa Mungu

Zuchu Asema Hatima ya Ndoa Yake na Diamond Ipo Mikononi mwa Mungu

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu, amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa kauli yenye utata kuhusu mustakabali wa uhusiano wake na staa wa muziki,Diamond Platnumz

Akihojiwa katika kipindi cha Refresh Show kinachorushwa na Wasafi TV, wakati wa hafla ya JP Night 2025, Zuchu alionesha wazi kuwa ndoa haipo kwenye mipango yake na Diamond, licha ya uhusiano wao wa muda mrefu ambao umeendelea kuibua gumzo mitandaoni.

Mkali huyo wa ngoma ya “Sukari” ameweka wazi kuwa hatima ya ndoa kati yake na mpenzi wake, Diamond Platnumz, haiko mikononi mwake bali yaachwe kwa Mwenyezi Mungu kuamua.

“Tumuachie Mungu, Atajua Wakati Sahihi na Mtu Sahihi.”, alisema Zuchu kwa utulivu,

Huku akionekana mwenye utulivu na kujiamini, Zuchu hakufafanua zaidi kuhusu hali halisi ya uhusiano wao, lakini maneno yake yameeleweka kama ishara ya kuwepo kwa mashaka au uwezekano wa mabadiliko katika safari yao ya kimapenzi.

Kauli hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki na wafuasi wa wawili hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifuatilia kwa karibu uhusiano wao wa kimapenzi. Wengi walitarajia kuwa mwaka huu huenda ungekuwa wa hatua kubwa kama uchumba au ndoa, lakini kauli ya Zuchu imeonyesha bado kuna sintofahamu.

Diamond Platnumz na Zuchu wamekuwa wakihusishwa kimapenzi kwa muda mrefu, ingawa mara kadhaa wamekana au kutoa majibu ya kujihami kuhusu uhusiano huo. Licha ya kuonekana pamoja mara kwa mara kwenye matamasha na hafla za kifamilia, bado hakuna uthibitisho rasmi wa ndoa au uchumba kutoka kwa wawili hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *