
Mwimbaji hodari wa Kike Tanzania Zuchu ametajwa kuwania tuzo za Kimataifa za MTVEMA kwa mwaka huu katika kipengele cha Msanii bora wa Afrika.
Katika kipengele hicho, Zuchu ambaye ndiye msanii pekee toka ukanda wa Afrika Mashariki kutajwa kuwania Tuzo hizo, atachuana na wasanii wengine wakubwa Afrika akiwemo Burna Boy, Tems, Ayra Starr, BlackSherif wa Ghana na Musa Keys.
Tayari dirisha la upigaji wa kura hizo limeshafunguliwa, na unaweza kuanza kupiga kura kupitia tovuti ya MTV EMA na hafla ya ugawaji wa tuzo hizo unatarajiwa kufanyika Novemba 13 mwaka huu huko Duesseldorf, Ujerumani.