Entertainment

Mashabiki waharibu mali ya thamani kubwa baada ya Gravity Omutujju kususia shoo

Mashabiki waharibu mali ya thamani kubwa baada ya Gravity Omutujju kususia shoo

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju ameingia tena kwenye headlines mara baada ya kususia moja ya onesho lake huko Lukaaya.

Duru za kkuaminika zinasema mashabiki walimsubiri pallaso kwa takriban masaa matatu lakini msanii huyo hakutokea kwenye performance yake, jambo lilowafanya mashabiki kuzua vurugu na kuaharibu kila kitu kwenye ukumbi wa burudani Royal Gardens  na kuacha mapromota wakikadiria hasara ya mamilioni ya pesa.

Juhudi za walinzi kuwatuliza mashabiki ziliambulia patupu kwani walionekana wenye hasira zaidi wakiwataka waliondaa onesho hilo kuwaregeshea pesa zao kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kumleta Gravity Omutujju jukwaani awape burudani.

Hata hivyo Mmiliki wa ukumbi wa Royal Gardens  ametaka usimamizi wa Kev Motors na Humble uliohusika kuandaa tamasha la Gravity Omutujju kulipia mali iliyoharibiwa ambayo thamani yake ni zaidi ya Shillingi 1.2m.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *