Others

Zuchu Awasihi Mashabiki Waamini Kazi Zao

Zuchu Awasihi Mashabiki Waamini Kazi Zao

Mwanamuziki nyota kutoka WCB Wasafi, Zuchu, ametoa ujumbe mzito kwa mashabiki na vijana wanaojitafuta kwenye sanaa na kazi zao, akiwahimiza waache kujihukumu kupita kiasi na badala yake waamini uwezo wao bila woga.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Zuchu amesema hakuna muda sahihi wa kufanya jambo, bali mtu anapaswa kuchukua hatua, kufanya kazi na kuondoa mawazo hasi yanayokatisha tamaa. Amesisitiza kuwa ubora wa kazi mara nyingi hutazamwa tofauti na mashabiki, hivyo kujikosoa kupita kiasi kunaweza kuua ndoto kabla hata ya kuanza.

Msanii huyo amefichua kuwa alipatwa na hofu kubwa kabla ya kuachia wimbo wake “Reason”, ambao aliimba kwa Kiingereza tofauti na mtindo wake wa kawaida. Zuchu amekiri kuwa aliwazia kuufuta kabisa wimbo huo kwa kuhofia ukosoaji na kuhisi kuwa ni kazi duni ambayo isingeweza kukubalika.

Hata hivyo, baada ya kumsikilizisha prodyuza wimbo huo, alipokea mrejesho mzuri, jambo lililomtia moyo zaidi na kuamua kuwashauri wengine wasikubali kushindwa na hofu au kujikosoa kupita kiasi.

Zuchu ametoa somo hilo akisema anaamini wengi hukwamishwa na mashaka yanayotokana na mawazo hasi, huku akisisitiza umuhimu wa kuamini safari na ubunifu wa mtu bila kuyumbishwa na hofu za ndani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *