Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize, ameingia studio kuandaa wimbo maalum unaolenga kuwatuliza na kuwapooza mioyo Watanzania kufuatia machafuko yaliyoshuhudiwa hivi karibuni nchini humo.
Kupitia Instastory yake, Harmonize ameposti video akiwa studioni akifanya mazoezi ya sauti kwa wimbo mpya ambao inadaiwa unaweza kuitwa “Don’t Be So Emotional”, kutokana na maneno aliyosikika akiimba katika moja ya video hizo.
Katika video nyingine, Harmonize ameonekana akiwa na Mbosso, hali iliyozidisha fununu kuwa huenda akamshirikisha mkali huyo wa ngoma ya Pawa kwenye mradi huo mpya.
Ingawa hajaweka wazi tarehe rasmi ambayo ataachia wimbo huo, dalili zinaonyesha kuwa Harmonize anaandaa kazi yenye kugusa hisia na kuleta faraja kwa wananchi waliokuwa na hofu na majonzi.