Mwanamuziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameonyesha moyo wa huruma baada ya kuahidi kumsaidia promota wa matamasha Biggie Events, aliyetupwa gerezani Luzira Prison kwa kushindwa kulipa deni la takriban Ugx milioni 70, sawa na takriban KSh milioni 2.5.
Kupitia mitandao ya kijamii, Spice Diana ameeleza kuguswa na hali ya promota huyo ambaye amekuwa akihangaika kurejesha mkopo aliouchukua kwa ajili ya kuandaa tamasha lililoshindwa kufanikiwa kibiashara.
Msanii huyo amesema yuko tayari kuchangia kiasi cha fedha ili kumsaidia Biggie kutoka gerezani, akiwataka pia wasanii na wadau wengine wa muziki nchini Uganda kuungana naye katika juhudi za kumsaidia promota huyo kurejea uraiani.
Biggie Events anafahamika kwa kuandaa matamasha kadhaa ya muziki nchini Uganda, yakiwemo yale yaliyowahi kumhusisha Spice Diana na wasanii wengine wakubwa.