Gossip

Kanyari Akosolewa kwa Kutumia Kifo cha Aliyekuwa Mke Wake Kutafuta Kiki

Kanyari Akosolewa kwa Kutumia Kifo cha Aliyekuwa Mke Wake Kutafuta Kiki

Mjadala mkali umeibuka mtandaoni baada ya mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii kumshutumu Mchungaji Victor Kanyari kwa kutumia kifo cha aliyekuwa mke wake, mwimbaji wa nyimbo za injili Betty Bayo, kama njia ya kutafuta kiki.

Taarifa hiyo imevutia hisia kali kutoka kwa Wakenya, wengi wakionesha kutoridhishwa na namna Kanyari ameonekana kujitokeza hadharani akionekana kulia na kushiriki kwa ukaribu katika maandalizi ya mazishi ya marehemu.

Mtandaoni, watumiaji wengi wameeleza kuwa kitendo hicho hakifai kwani Kanyari na Betty walishatalikiana miaka kadhaa iliyopita, na marehemu alikuwa ameolewa tena na mwanaume mwingine. Wengi wamesema kuwa hatua ya Kanyari kuonekana kana kwamba anaongoza kamati ya mazishi inamvunjia heshima mume wa sasa wa marehemu.

Mjadala huu umeendelea kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao, huku baadhi wakimtetea Kanyari wakisema ana haki ya kuomboleza kwa sababu walishiriki maisha na watoto pamoja, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa kumpa familia nafasi ya kupanga mazishi kwa utulivu na heshima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *