Entertainment

Kizz Daniel Avunja Ukimya Baada ya Vurugu Kwenye Show Yake Paris

Kizz Daniel Avunja Ukimya Baada ya Vurugu Kwenye Show Yake Paris

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Kizz Daniel, amevunja ukimya kufuatia madai ya kuchelewa kufika kwenye onyesho lake lililofanyika jijini Paris, Ufaransa, jana, hatua iliyosababisha vurugu kati ya mashabiki na waandaaji wa tamasha hilo.

Kupitia Insta story yake, Kizz Daniel amekanusha madai kuwa yeye ndiye chanzo cha kuchelewa, akieleza kuwa tatizo lilitokana na mgogoro wa kibiashara kati ya wakala wa ziara yake Olamide Baron na mpangaji wa tamasha hilo.

Msanii huyo amesema kuwa alilipwa kikamilifu na Olamide Baron kwa ajili ya kutumbuiza Paris, lakini wakala huyo aliuza show kwa promota mwingine ambaye, kwa mujibu wa Kizz Daniel, alivunja mkataba kwa kushindwa kumlipa fedha zake ipasavyo.

Kizz Daniel pia amefafanua kuwa alikuwa tayari kwa safari tangu saa 12:00 asubuhi kwa ajili ya ndege ya saa 6:25 mchana, akiwa hotelini na kaka yake Adesope, lakini ndege hiyo ilicheleweshwa ili wakala wake aweze kulipwa kwanza. Kufuatia ucheleweshaji huo, walikosa ndege ya awali na kulazimika kusubiri ndege nyingine iliyondoka saa 11:25 jioni, hali iliyosababisha kufika Paris kwa kuchelewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *