Entertainment

Harmonize Ampongeza Davido kwa Kuwakumbuka Watanzania Waliofariki kwenye Machafuko ya Uchaguzi

Harmonize Ampongeza Davido kwa Kuwakumbuka Watanzania Waliofariki kwenye Machafuko ya Uchaguzi

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameonekana kuguswa na kitendo cha msanii wa Nigeria Davido kusimamisha tamasha lake nchini Marekani ili kutoa heshima kwa Watanzania waliofariki wakati wa machafuko ya uchaguzi ya Oktoba 29.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amepongeza hatua hiyo, akitoa wito wa maombi ya pamoja kwa nchi za Tanzania, Sudan Kusini, Nigeria na Afrika kwa ujumla, ili amani itawale na waliopoteza maisha wapumzike kwa amani.

Harmonize ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa maendeleo ya Albamu yake mpya 31 ambayo kwa mujibu wake huenda ikakosa kutoka mwaka huu kutokana na sababu ambazo hakuziweka wazi. Mkali huyo wa ngoma ya Best Friend, amesema kwa sasa ameanzisha mchakato wa mazungumzo na uongozi wake kuhusu mipango ya kuachia kazi hiyo mwaka 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *