Entertainment

KRG The Don Akanusha Kufulia Kiuchumi

KRG The Don Akanusha Kufulia Kiuchumi

Msanii na mfanyabiashara KRG The Don amejitokeza hadharani kupinga uvumi unaosambaa mtandaoni kwamba amefulia kiuchumi, akisisitiza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

Kuptia video aliyochapiha mtandaoni, KRG amesema kuwa utajiri wake si wa kubahatisha, bali umetokana na kazi zake nyingi alizofanya kwa muda mrefu katika muziki, biashara na uwekezaji mbalimbali.

Msanii huyo, amesisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kufuta utajiri wake, kwani ni mtu aliyebarikiwa tangu zamani na ambaye ameendelea kujijenga kupitia juhudi zake.

KRG pia amewataka wakosoaji wake kuacha kumhusisha na umaskini, akisema kuwa alizaliwa katika mazingira yenye uwezo na ataendelea kuishi maisha ya kifahari aliyoyatengeneza mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *