Mwanamitandao na content creator Pritty Vishy ameendelea kufunguka kuhusu safari yake ya kujikubali, akielezea kwa uwazi kwamba alipitia kipindi kigumu cha kutokuwa na uthamini binafsi.
Akiangazia maisha yake ya nyuma, Pritty amesema kwamba wakati fulani alihisi kuwa mwanamume hansome akimchumbia, basi alikuwa akimfanyia fadhila.
Katika ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Pritty Vishy ameeleza kuwa mawazo hayo yalitokana na kujichukia kupita kiasi na kukosa kujiamini. Hata hivyo, amesisitiza kuwa sasa yuko katika hatua mpya ya maisha, ambapo anajipenda, anajiheshimu na hatakubali mtu yeyote kumshusha tena.
Mrembo huyo amesema kuwa safari yake ya kukuza kujiamini na kujiweka mbele imekuwa ya muhimu sana katika kumjenga kama mwanamke anayejua thamani yake. Kwa sasa, amesisitiza kuwa hakuna mtu anayeweza kumwambia chochote kitakachomrudisha kwenye hali ya kujionea huruma aliyopitia zamani.