Tech news

WhatsApp Yaboresha Groups kwa Kipengele cha Kuona Chats Zilizopita

WhatsApp Yaboresha Groups kwa Kipengele cha Kuona Chats Zilizopita

Kampuni ya WhatsApp imetangaza mabadiliko mapya kwenye huduma yake ya makundi (groups), hatua inayolenga kuboresha uzoefu wa watumiaji wanapojiunga na makundi mapya.

Katika maboresho mapya yaliyotangazwa, sasa mtumiaji atakapoongezwa kwenye group ataweza kuona baadhi ya ujumbe uliotumwa kabla ya kujiunga kwake.

Kwa kawaida, mtumiaji anapojiunga kwenye group kwa mara ya kwanza, hakuwa na uwezo wa kuona ujumbe (chats) zilizotumwa kabla ya yeye kuongezwa. Hali hii mara nyingi ilisababisha changamoto ya kushindwa kuelewa mjadala unaoendelea au muktadha wa mazungumzo ya awali.

Kwa mujibu wa utaratibu huo mpya, mtu anayekuongeza kwenye group atakuwa na uwezo wa kuchagua idadi ya ujumbe wa awali utakaoonekana kwa mwanachama mpya. Idadi hiyo inaweza kuwa kati ya ujumbe 25 hadi 100 zilizopita kabla ya kujiunga kwake.

Hatua hii inalenga kusaidia wanachama wapya kufahamu mwelekeo wa mjadala unaoendelea, mada inayojadiliwa pamoja na maamuzi yaliyofikiwa kabla ya wao kujiunga. Hivyo, itarahisisha ushiriki wao na kuwapa nafasi ya kuchangia hoja kwa uelewa mpana zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *