Tech news

Instagram Yaleta Option Mpya ya Kubadilisha Cover ya Post Kwenye Profile

Instagram Yaleta Option Mpya ya Kubadilisha Cover ya Post Kwenye Profile

Mtandao wa kijamii wa Instagram umeongeza option mpya inayoruhusu watumiaji kubadilisha mwonekano wa cover ya post inavyoonekana kwenye profile yao.

Kwa muda mrefu, watumiaji wa Instagram walikuwa na uwezo wa ku-edit thumbnail au cover ya video za Reels pekee. Hata hivyo, option hiyo haikuwepo kwa post za picha za kawaida kwenye profile; ilikuwa inapatikana kwa video tu.

Kupitia sasisho hili jipya, watumiaji sasa wanaweza kuchagua cover ya post zao ili kuamua ni sehemu gani ya picha itaonekana kwenye profile grid. Hii inawapa uhuru zaidi wa kupanga na kuboresha muonekano wa profile yao.

Ili kubadilisha cover ya post, nenda kwenye profile yako ya Instagram, bonyeza na ushikilie (hold) kwenye post unayotaka kubadilisha, kisha chagua option ya β€œAdjust Preview.” Kupitia option hiyo utaweza kusogeza au kupanga upya sehemu ya picha itakayoonekana kwenye profile yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *