Sports news

Arsenal Yaendelea Kuchanja Mbuga Kileleni mwa EPL

Arsenal Yaendelea Kuchanja Mbuga Kileleni mwa EPL

Klabu ya Arsenal imeendeleza kasi yake ya kusaka taji la Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuibuka na ushindi muhimu wa 1-0 dhidi ya Brighton & HoveAlbion katika uwanja wa Amex. Bao la pekee la mshambuliaji Bukayo Saka katika dakika ya 9 lilitosha kuwapa Gunners alama tatu muhimu na kuongeza mwanya wa uongozi kileleni kufikia alama saba.

Wakati Arsenal ikisherehekea, mahasimu wao Manchester City walipoteza alama muhimu nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Nottingham Forest. City walitangulia kwa mabao ya Antoine Semenyo na  Rodri lakini Forest walipambana na kusawazisha kupitia Morgan Gibbs-White na Elliot Anderson, matokeo yaliyowaacha mabingwa hao watetezi wakiwa nyuma kwa alama saba dhidi ya Arsenal.

Katika mechi nyingine zilizopigwa jana usiku, Chelsea walipata ushindi mnono wa 4-1 ugenini dhidi ya Aston Villa, huku João Pedro aking’ara kwa kufunga hat-trick.Newcastle United waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester United katika dimba la St. James’ Park. West Ham United waliondoka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Fulham ugenini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *