Rapa kutoka Kenya Femi One ametoa tahadhari kwa marapa wa kike nchini humo akiwataka kuepuka kumhusisha kwenye mabishano au bifu zao za kimuziki.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Femi One amesema yeye pamoja na rafiki yake wa karibu Wangechi hawataki kutajwa kwenye migogoro ya wasanii wengine, akisisitiza kuwa wanajua vyema uwezo wao kwenye rap na hawahitaji kuthibitisha chochote.
βSisi waschana tunajua ku-rap ata hatuna mambo, tunangoja tu mtutaje kuwake,β aliandika Femi One kwa utani lakini pia akionyesha kuwa wako tayari iwapo watahusishwa kwenye mzozo wowote wa kimuziki.
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo bifu kati ya Dyana Cods na Maandy limeendelea kushika kasi mitandaoni. Wasanii hao wawili wamekuwa wakirushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii huku kila mmoja akijinasibu kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuandika na kurap