Mwanamitandao na mke wa mwanamuziki Bahati, Diana Marua, ametoa onyo la utani lakini lenye ujumbe mzito kwa wanawake wanaodaiwa kumvamia mtoto wake, Morgan Bahati, kwenye ujumbe wa moja kwa moja (DMs).
Diana amefichua kuwa tangu Morgan apewe simu mpya ya iPhone 17, akaunti zake za mitandao ya kijamii zimefurika ujumbe kutoka kwa wanawake wanaotaka namba yake ya simu. Kwa mujibu wa Diana, zaidi ya ujumbe 1,000 umetumwa na wanawake wanaotaka kuwasiliana na kijana huyo.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Diana amesema wanawake hao wanapaswa kumpa Morgan nafasi kwa sababu bado ni mdogo sana.
Diana ameongeza kuwa ingawa anafurahia kuona mwanawe akipendwa na watu wengi, bado anasisitiza kuwa Morgan ana safari ndefu mbele yake na anahitaji muda wa kukua bila presha kutoka kwa watu.
Morgan, ambaye mara nyingi huonekana kwenye mitandao ya kijamii ya wazazi wake, amekuwa akivutia mashabiki wengi kutokana na tabia yake ya upole na uhusiano wa karibu na familia ya Bahati.