Entertainment

Eminem ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hiphop – 50 Cent

Eminem ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hiphop – 50 Cent

Rapa 50 Cent hakubaliani na hoja isemayo kwamba Jay-Z ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hip Hop kuliko Eminem. 50 Cent ameipinga hoja hiyo ambayo imesemwa na nyota wa zamani wa NBA, Jamal Crawford kwenye podcast ya Shaquille O’Neal, 50 Cent alishuka kwenye comment na kusema ni upuuzi mtupu.

Sio mara ya kwanza kwa 50 Cent kumkingia kifua Eminem hasa pale inapokuja mijadala mizito ya muziki wa Hiphop, itakumbukwa Oktoba 2022 kwenye mahojiano na Ebro in The Morning, 50 Cent alisema “Rap God” Eminem hapewi heshima ambayo anastahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *