Entertainment

Harmonize Aendelea Kuumia Kimapenzi, Aandika Machungu Snapchat

Harmonize Aendelea Kuumia Kimapenzi, Aandika Machungu Snapchat

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Harmonize, anaonekana kupitia kipindi kigumu upande wa mahusiano licha ya kuwa na jina kubwa kwenye tasnia ya muziki na utajiri wa kutosha. Kupitia akaunti yake ya Snapchat, Harmonize amemwaga hisia zake kwa uchungu kuhusu mpenzi wake ambaye bado hajawa tayari kumkubali kikamilifu kwenye maisha yake.

Katika ujumbe wake, Harmonize alieleza kwa wazi kwamba ana mapenzi ya dhati kwa mwanamke huyo, na kwamba siku atakayokubali kuwa naye rasmi, atamuoa papo hapo bila kuchelewa. Hata hivyo, kwa sasa ameamua kumpa nafasi ya kuendelea na maisha yake huku yeye akiendelea kumsubiri kwa subira.

“Mimi ni mtu mzima, niko tayari. Siku akiamua tu, sihitaji hata kupanga… nitamuoa siku hiyohiyo,” aliandika Harmonize kwa hisia kali.

Mashabiki wengi wameonesha hisia tofauti, wengine wakimpongeza kwa uvumilivu na upendo wa kweli, huku wengine wakimshauri asijidhalilishe kwa mapenzi yasiyolipwa kwa kiwango sawa.

Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kulalamika kuhusu changamoto za kimapenzi, jambo ambalo limezua mijadala mitandaoni kuhusu maisha ya mahusiano ya wasanii mashuhuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *