Entertainment

“Bora Nife Nikapumzike…” – Yamii Aandika Ujumbe wa Kushtua Instagram

“Bora Nife Nikapumzike…” – Yamii Aandika Ujumbe wa Kushtua Instagram

Msanii chipukizi wa muziki wa Bongo, Yamii, ameibua hofu mitandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kusikitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza hali ya kukata tamaa na msongo wa mawazo, kabla ya kuufuta muda mfupi baadaye.

Katika ujumbe huo, Yamii alielezea hali ya kuchoka kimaisha na kusema kuwa haoni tena sababu ya kuendelea kuishi, akionesha kuwa amefikia kikomo cha uvumilivu wake. Aliomba msamaha kwa wazazi wake, ndugu na mashabiki, akionekana kubeba huzuni kubwa moyoni. Aliitaja pia msanii mwenzake Nandy, akimwomba radhi iwapo aliwahi kumkosea.

“Mashabiki zangu naombeni mniombee. Msamaha kwa mama angu na baba angu na baba yangu. Mimi ndio tegemeo lakini naona siwezi kuishi tena. Nimechoka, bora nife nikapumzike. Naombeni msamaha kwa wote wote niliowahi kuwakosea. Mimi basi tena nimefika mwisho, siwezi tena, bora nikapumzike. Siwezi tena siwezi tena walahi siwezi… @officialnandy pia dada angu naomba nisamehe popote niliwahi kukukosea,” Aliandika kwa hisia kali

Ujumbe huo ulisambaa kwa kasi mitandaoni, huku mashabiki na watu maarufu wakieleza kusikitishwa na hali hiyo. Wengi walihoji hali ya afya ya kiakili ya msanii huyo na kutoa wito kwa watu wa karibu naye kumsaidia haraka.

Baada ya ujumbe huo kufutwa, mjadala uliendelea kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakianza kampeni ya kumwombea na kumtia moyo kwa hashtag kama #PrayForYamii na #MentalHealthMatters. Wengine walitoa wito kwa wasanii wenzake, familia na mashabiki kuwa karibu naye ili kumsaidia kupitia kipindi hiki kigumu.

Hadi kufikia sasa, Yamii hajatoa kauli yoyote rasmi kuhusu ujumbe huo, na haijafahamika hali yake ya sasa. Mashabiki na wadau wa burudani wanaendelea kufuatilia kwa makini