LifeStyle

Baby Mama wa Bahati Avishwa Pete ya Uchumba na Mwanaume wa Ndoto Yake

Baby Mama wa Bahati Avishwa Pete ya Uchumba na Mwanaume wa Ndoto Yake

Baby Mama wa mwanamuziki Bahati, Yvette Obura, ametangaza rasmi kuwa amevishwa pete ya uchumba na mwanaume anayemuita zawadi kutoka kwa Mungu.

Kupitia video aliyoshiriki mtandaoni, Yvette amesema amekubali kuolewa na mwanaume aliyemfanya aamini tena katika upendo, akisema kuwa baada ya kupitia maumivu ya zamani na mahusiano yaliyoshindikana, sasa ameona upendo wa kweli.

Mama huyo wa mtoto mmoja, ameeleza kuwa mwanaume huyo amemsaidia kuona maana halisi ya upendo wa dhati, na kwamba anaamini ndiye mtu sahihi aliyepangwa kwake na Mungu.

Yvette anayefahamika kama Mama Mueni, amesema safari yake ya kimapenzi imekuwa ndefu na yenye changamoto nyingi, lakini sasa ana amani, furaha na matumaini mapya kuhusu maisha ya ndoa.

Taarifa hiyo imepokelewa kwa furaha na mashabiki wengi mitandaoni, waliompongeza kwa kuanza ukurasa mpya wa maisha, huku wakimtakia baraka na upendo wa kudumu katika safari yake mpya ya ndoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *