Gossip

Noti Flow Asema Wafuasi Laki 2 Walimkimbia Baada Kukataa Uchumba wa Mustafa

Noti Flow Asema Wafuasi Laki 2 Walimkimbia Baada Kukataa Uchumba wa Mustafa

Msanii wa muziki kutoka Kenya Noti Flow amefunguka kuhusu jinsi ombi la ndoa la ghafla kutoka kwa msanii mwenzake Colonel Mustafa lilivyotikisa maisha yake binafsi.

Kupitia instastory yake, Noti Flow amesema tukio hilo, lililotokea hadharani kwenye kipindi cha Obinna TV Live, lilipelekea kuvunjika kwa uhusiano wake wa wakati huo pamoja na kupoteza zaidi ya wafuasi 200,000 kwenye mitandao ya kijamii.

Mrembo huyo amesema mashabiki wengi walitafsiri tukio hilo vibaya, wakidhani amemdhalilisha Mustafa kwa kukataa ombi hilo hadharani, jambo lililompa changamoto kubwa kwenye maisha yake ya kisanaa na kibinafsi.

Noti Flow ametoa wito kwa mashabiki kuzingatia hali za mtu binafsi kabla ya kutoa maoni mtandaoni, huku akisisitiza umuhimu wa heshima na nafasi ya kila mmoja kuamua katika maisha ya mapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *