LifeStyle

Msanii Chosen Becky Adokeza Mpango wa Kuzaa Watoto 12

Msanii Chosen Becky Adokeza Mpango wa Kuzaa Watoto 12

Mwanamuziki nyota kutoka nchini Uganda, Chosen Becky, amefichua mipango yake ya kuwa na familia kubwa yenye watoto kumi na wawili au zaidi, akisema ni ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

Akipiga stori na Youtuber mmoja nchini humo, Becky amesema anapenda sana watoto na anaamini Mungu atampa nguvu ya kutimiza ndoto hiyo ya kuwa mama wa familia kubwa. Ameongeza kuwa kwa sasa anafurahia ndoa yake, akisema mume wake amempa maisha mapya yaliyojaa amani na furaha, na kumsaidia kung’aa zaidi kimwonekano na kimaisha.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Let it Rain, pia amefichua kuwa yeye na mpenzi wake Sekajja wanapanga kufunga ndoa rasmi hivi karibuni kabla ya kuanza kupanua familia yao.

Hata hivyo, Becky amesisitiza kuwa ana imani na mipango ya Mungu na kwamba ataendelea kulea familia yake kwa upendo na nidhamu bila kujali ukubwa wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *