Mhubiri Victor Kanyari ameibua hisia nzito leo wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Betty Bayo, akitoa hotuba ya kuonyesha masikitiko yake pamoja na kumwomba msamaha kwa yaliyowahi kutokea kati yao wakati wa uhai wake.

Kanyari ametumia muda huo muhimu kueleza kuwa drama na changamoto zilizozikumba maisha yao ya awali zilimfanya Betty kupitia wakati mgumu, jambo ambalo leo analiona kama doa ambalo halikupaswa kumwangukia. Amemtaja marehemu Betty kama mwanamke mchapakazi, mwenye moyo wa kusamehe, mama mwenye upendo na rafiki wa kweli ambaye aliwahi kuwa sehemu muhimu ya maisha yake.

Katika hotuba yake, amesisitiza kwamba licha ya changamoto walizowahi kushuhudia kwa pamoja, Betty alibaki kuwa mtu wa amani, hekima na aliyejitolea kuwalea watoto na kuendeleza huduma yake ya muziki wa injili bila kuyumbishwa.

Mazishi ya marehemu Betty Bayo yalifanyika leo katika eneo la Mugumo Estate, Kaunti ya Kiambu, ambako familia na marafiki wa karibu walimpumzisha kwenye nyumba yake ya milele baada ya kutoa heshima zao za mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *