Gossip

Diamond Aingilia Ndoa ya Mwijaku

Diamond Aingilia Ndoa ya Mwijaku

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameamua kuingilia kati sakata la ndoa ya mtangazaji na mwanahabari Mwijaku, ambayo kwa sasa inadaiwa kuyumba kufuatia madai ya usaliti.

Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Diamond ameonekana akiwa pamoja na Mwijaku ambapo alitumia fursa hiyo kumuomba msamaha mke wa Mwijaku na kumshawishi arejee nyumbani ili kuokoa ndoa yao.

Diamond amemhimiza Mwijaku kutatua tofauti zilizopo kati yake na mkewe badala ya kufikiria kuachana, akisisitiza kuwa ndoa inahitaji uvumilivu na msamaha. Ameeleza kuwa mke wa Mwijaku ni mtu wa thamani ambaye wameishi naye kwa amani kwa muda mrefu, hivyo haifai kuvunja ndoa kwa sababu ya changamoto.

Akizungumza kwa hisia, Diamond amesisitiza kuwa wamepitia kipindi kigumu sana kama familia na marafiki, na akaomba kwa unyenyekevu mke wa Mwijaku amsamehe mumewe kwa ajili ya mustakabali wa familia yao.

Hatua hiyo ya Diamond imekuja baada ya mke wa Mwijaku kuripotiwa kumkimbia mumewe, hali iliyozua gumzo kubwa mitandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *