Staa wa muziki kutoka Kenya, Bien Aime Baraza, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa anamiliki fahali anayejulikana kwa jina la Sauti Sol.
Kupitia maelezo yake, Bien amesema awali alikuwa na fahali wawili, lakini mmoja aliuziwa na mama yake mzazi, na hivyo kubaki na fahali mmoja ambaye alimpa jina hilo linalofanana na kundi lake la muziki.
Bien ameeleza kuwa kwa sasa fahali huyo ameanza kupewa mafunzo maalum ya kupigana na fahali wengine, ikiwa ni maandalizi ya kushiriki mashindano ya kupiganisha fahali. Mashindano hayo yanajulikana kudhaminiwa na jamii ya Waluhya, hasa kutoka Kaunti ya Kakamega nchini Kenya, na ni sehemu ya tamaduni na burudani za kitamaduni katika eneo hilo.
Hata hivyo, Bien amesema amesema anajivunia fahali wake na ana matumaini kuwa “Sauti Sol” itafanya vyema endapo itashiriki mashindano hayo, huku akisisitiza kuwa anathamini na kuheshimu tamaduni ya Waluhya ambayo ndio chimbuko lake