Msanii wa muziki kutoka Kenya, Nadia Mukami, ameshindwa kuficha furaha yake baada ya wimbo wake mpya Woza kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya YouTube Trending Kenya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nadia amewashukuru mashabiki wake pamoja na Mungu kwa mafanikio hayo makubwa, akieleza kuwa mapenzi na sapoti ya mashabiki ndiyo yameufikisha wimbo huo kileleni kwa muda mfupi.
Katika ujumbe wake, Nadia pia ametangaza kuwa ataandaa “dera party” Ijumaa hii kusherekea mafanikio ya Woza. Amewaalika mashabiki wake kupendekeza sehemu nzuri itakayofaa kufanyika sherehe hiyo, akisema angetamani kusherekea pamoja nao.
Video ya wimbo Woza iliachiwa rasmi Disemba 11, na ndani ya siku nne pekee tayari imefanikiwa kukusanya zaidi ya views laki tatu kwenye YouTube, jambo linaloonesha ukubwa wa mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wake.