Sports news

West Ham Yamnasa Adama Traore Kutoka Fulham kwa Pauni Milioni 2

West Ham Yamnasa Adama Traore Kutoka Fulham kwa Pauni Milioni 2

Kilabu cha West Ham kimemsajili winga Adama Traore kutoka Fulham kwa ada ya pauni milioni 2. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anahama kutoka magharibi hadi mashariki mwa London, ambapo anaungana tena na Nuno Espirito Santo, ambaye alimsimamia katika Wolves.

Mchezaji huyo amabye ameichezea uhispania mechi nane, ameanza mechi mbili pekee za Ligi kuu timuni Fulham msimu huu na hakuhusika katika ushindi wao wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Brighton Jumamosi. Mechi ya mwisho ya Traore akiwa Fulham ilikuwa katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Middlesbrough kwenye Kombe la FA tarehe 10 Januari.

Traore aliwahi kucheza timu za Aston Villa, Middlesbrough na Wolves kabla ya kujiunga na Fulham mwaka 2023 kwenye uhamisho wa bure. West Ham bado iko katika eneo la kushushwa daraja msimaoni ikiwa na alama 20, tano nje ya usalama licha ya kushinda mechi zao mbili zilizopita za ligi, huku kukiwa kumesalia mechi 15 kuchezwa msimuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *