Entertainment

Alien Skin Atoa Onyo Kali kwa Wafuasi wa NUP

Alien Skin Atoa Onyo Kali kwa Wafuasi wa NUP

Msanii mwenye utata nchini Uganda, Alien Skin, ametoa onyo kali kwa wafuasi wa chama cha National Unity Platform (NUP) akiwataka waache kumshambulia mitandaoni.

Akizungumza kupitia TikTok Live, Alien Skin amesema kuwa yuko kwenye level moja na kiongozi wa chama hicho, Bobi Wine ikizingatiwa kuwa ana ushawishi mkubwa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii huyo amesisitiza kuwa anastahili heshima, kutambuliwa na kuungwa mkono kama ilivyo kwa Bobi Wine, akieleza kuwa ana wafuasi wengi na nguvu ya kuwavuta vijana katika maeneo mbalimbali ya Uganda.

Kwa takribani miaka miwili sasa, Alien Skin amekuwa katika mvutano wa mara kwa mara na wafuasi NUP, hali iliyojaa maneno makali na mabishano kwenye majukwaa mbalimbali ya kijamii. Inadaiwa kuwa mzozo huo ulianza baada ya msanii huyo kujitenga na kambi ya upinzani na kuonyesha wazi kumuunga mkono chama tawala cha NRM, hatua iliyowakasirisha pakubwa wafuasi wengi wa NUP.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *