Content creator kutoka Kenya, Dem wa Facebook amekataa kuweka wazi jina la mwanaume aliyempa ujauzito baada ya mashabiki kuendelea kumuuliza ni nani baba wa mtoto anayemtarajia.
Kupitia mitandao ya kijamii, Dem wa Facebook amesema ujauzito wake ni jambo la binafsi na hahitaji kuthibitisha au kueleza chochote kwa umma licha ya umaarufu wake mitandaoni.
Mrembo huyo, ameeleza kuwa anachochagua kushiriki ni maisha yake binafsi kwa kiwango anachokiona kinafaa, na si kila kitu lazima kiwekwe hadharani.
Kauli yake imekuja mara baada ya kuwataarifu mashabiki zake kuwa anatarajiwa kupata mtoto hivi karibuni, taarifa iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni. Hata hivyo, licha ya pongezi kutoka kwa baadhi ya mashabiki, wapo watu waliotilia shaka madai hayo na kudai huenda ni njia ya kuvutia hisia za umma.