Msanii wa kimataifa kutoka Afrika Kusini, Tyla, ameendelea kuandika historia katika muziki wa Afrika baada ya kutwaa tuzo ya Grammy kupitia wimbo wake “Pusha 2 Start” katika kipengele cha Best African Performance.
Tyla aliwashinda wasanii wakubwa barani Afrika akiwemo Davido, Ayra Starr aliyeshirikiana na WizKid katika wimbo “Gimmie Dat”, Burna Boy kupitia wimbo “Love”, pamoja na Eddy Kenzo aliyeshirikiana na Mehran Matin katika wimbo “Hope & Love”.
Ushindi huu unamweka Tyla kwenye vitabu vya historia kama msanii wa kwanza kushinda kipengele cha Best African Performance mara mbili mfululizo.
Mwaka 2024, Tyla alitwaa tuzo hiyo kupitia wimbo wake uliotikisa dunia, “Water”, uliomfungulia milango ya soko la kimataifa.