Gossip

WILLY PAUL ATISHIA KUMCHUKULIA DIANA MARUA HATUA KALI ZA KISHERIA

WILLY PAUL ATISHIA KUMCHUKULIA DIANA MARUA HATUA KALI ZA KISHERIA

Mwanamuziki willy paul  amehapa kumchukulia hatua kali za kisheria Diana Marua,baada mrembo huyo ya kudai kuwa alijaribu kumbaka miaka michache iliyopita.

Katika taarifa kwenye mtandao wa Instagram, Pozze amesema kuwa atamshtaki Diana Marua kwa madai ya kumharibia jina huku akidai kwamba hasimu wake wa muda mrefu Bahati anamtumia mke wake kumshusha kimuziki.

Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema tuhuma za kujaribu kumubaka Diana Marua hayana msingi wowote na yamepangwa ili mrembo huyo apate huruma kutoka kwa umma kama njia ya kusukuma muziki wake uwafikie wengi.

Hata hivyo Willy Paul amesisitiza kuwa hajawahi kumlazimisha au kushiriki ngono na mtu yeyote bila maelewano huku akikiri kuwa na msongo wa mawazo baada ya aliyekuwa msanii wake miss p kumhutuma kuwa alimnyanyasa kimapenzi.

Kauli ya mtu mzima Willy Paul imekuja mara baada ya mke wa Bahati, Diana B kupitia Youtube Channel yake kuibua madai kwamba kuna kipindi bosi huyo Saldido alimrubuni na kisha akamnyanyasa kingono.

Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kuhapa kumpeleka mahakamani Willy Paul kwa kuwa ni wanawake wengi aliowafanyia ukatili huo na kwamba ni lazima awamu hii sheria ichukue mkondo wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *