Entertainment

Diamond Platnumz Aweka Rekodi Nyingine Dodoma Kwa Kuijaza Chinangali Park

Diamond Platnumz Aweka Rekodi Nyingine Dodoma Kwa Kuijaza Chinangali Park

Msanii wa kimataifa kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ameendelea kuthibitisha ubora wake katika tasnia ya muziki baada ya kuweka rekodi nyingine kubwa jijini Dodoma kwa kufanikiwa kujaza uwanja wa wazi wa Chinangali Park.

Katika tukio hilo lililovutia maelfu ya mashabiki, Diamond aliweza kuujaza uwanja huo huku viingilio vikianzia shilingi 70,000 hadi kufikia shilingi milioni 5 kwa sehemu za VIP, jambo linaloonesha nguvu yake kubwa ya ushawishi na mapenzi makubwa aliyonayo kutoka kwa mashabiki wake.

Show hiyo iligeuka kuwa gumzo jijini Dodoma, ambapo mashabiki walifurika mapema kuhakikisha wanapata nafasi ya kushuhudia burudani kutoka kwa nyota huyo wa Bongo Fleva anayetikisa kimataifa. Diamond alitumbuiza kwa nguvu, akiimba nyimbo zake maarufu zilizowafanya mashabiki kuimba sambamba naye kuanzia mwanzo hadi mwisho wa show.

Mafanikio hayo yanaingia kwenye orodha ndefu ya rekodi ambazo Diamond Platnumz ameendelea kuweka ndani na nje ya Tanzania, akithibitisha kuwa bado anaendelea kuwa mmoja wa wasanii wakubwa zaidi barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *