
Mchekeshaji Eric Omondi ameingia kwenye headlines baada ya kutaka kuzichapa na member wa Sauti Sol, Bien baraza usiku wa kuamkia Januari mosi katika onesho la Konshens Jijini Nairobi.
Chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Omondi kushinikiza kundi la Sauti Sol watumbuize wa mwisho katika orodha ya wasanii kama njia ya kuwapa heshima.
Làkini Pia Bien katika moja ya interview amenukuliwa akisema muda wanaopewa kuperfom kama kundi la Sauti Sol katika tamasha haijawahi kuwa tatizo kwao, iwapo atakuwa wasanii wa kwanza au wa mwisho katika orodha ya wasanii.
Ikumbukwe kwa muda sasa eric omondi amekuwa akipaza sauti juu ya wasanii wa kenya kutotendewa haki na waandaaji wa matamasha ya muziki.
Hii ni baada ya wasanii wa mataifa mengine kuonekana kupewa kipau mbele kufanya shows nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.