Gossip

KHADIJA KOPA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU ISHU YA DIAMOND KUTOKA KIMAPENZI NA ZUCHU

KHADIJA KOPA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU ISHU YA DIAMOND KUTOKA KIMAPENZI NA ZUCHU

Moja kati ya headlines zinazo gonga vichwa vya habari mtandaoni ni issue inayomtaja mwanamuziki diamond platnumz kutaka kumuoa mwanamuziki mwenzake zuchu , sakata ambalo kila mtu analizungumzia katika namna yake.

Sasa mama mzazi wa zuchu, Khadija Kopa amezungumzia kile kinachoitwa penzi jipya mtandaoni kati ya binti yake, Zuchu na Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano Kopa  ambaye ni Malkia wa muziki wa Taarab nchini tanzania amepuuzilia mbali madai hayo na kusema aliwasiliana na bintiye na akamueleza hali halisi kuwa huo ni uvumi tu usio na msingi.

Zuchu alimhakikishia mama yake kuwa Diamond amekuwa akimuonyesha heshima kubwa na hakuna chochote kinachoendelea kati yao.

“Wakati ule Zuhura aliniambia Diamond anamheshimu sana na hajawahi hata siku moja kuniambia vitu vya kipuzi. Nilishtuka maanake watu walikuwa wanavumisha kupita kiasi” amesema na kuongeza;

“Nilishangaa mbona walivumisha kupita kiasi, mimi mwenyewe sikushughulika sana, nilimuuliza Zuhura mbona watu walivumisha sana ama kuna kitu chochote. Aliniambia hamna wala hajawahi kuvunjiwa heshima hata siku moja, mimi nilichukulia kama kitu cha kawaida” alisema Khadija Kopa.

Aliendelea kwa kusema; “Diamond mimi ananiona kama mama yake kusema ukweli, tangu zamani, kabla hata huyo Zuchu hajaenda Wasafi, amenichukulia kama mama yake”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *