
Mwanamuziki wa nyimbo za injili ringtone ameshika vichwa vya habari wikiendi hii iliyopita mara baada ya kutaka kuzichapa na DJ Mo ambaye mume wa msaniii mwenzake Size 8.
Purukushani kati ya wawili hao ilianza baada ya ringtone kuzua vurugu kwenye hafla ya uzinduzi wa album ya msanii size 8 ambayo imefanyika Februari 13 mwaka huu kwa kutaka kujiunga na wahubiri waliopewa nafasi ya kuibariki album ya size 8, Christ Revealed kabla ya kuingia sokoni.
Sasa suala hilo lilimlazimu mume size 8, DJ MO kutumia nguvu kumuondoa ringtone kwenye eneo la tukio kutokana na msanii huyo kutaka kuaharibu hafla ya uzinduzi wa album size 8 kwa kusisitiza kujiunga na wachungaji kwa lazima.
Akizungumza nje ya hafla ya uzinduzi wa album size 8 ringtone amesema ameshangazwa na hatua ya DJ Mo kumkataza kujiunga na wahubiri wenzake stejini kuiombea album huku akimsuta vikali kwa hatua ya kumvunjia heshima mbele ya umma licha ya kuwa msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini.
Kwa upande wake DJ MO amepuzilia mbali madai ya ringtone kwa kusema kwamba hayana msingi wowote kwani msanii huyo anapenda kuleta mzaha kwenye shughuli za watu hivyo hangemruhusu kuaharibu hafla ya uzinduzi wa album ya mke wake Size 8.
Hata hivyo jambo hilo limezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwani walimwengu wameonekana kumshambulia ringtone kwa hatua kuvuruga shughuli ya yenyewe huku wengine wakihoji kuwa huenda msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwa ajili ya wimbo wake na size 8 ambao unapatikana kwenye Christ Revealed album