
Aliyekuwa msanii wa Magix Empire, Rudra Kartel amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha yake kwa kusema kwamba alitupwa jela kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Katika mahojiano na Plugtv Rudra amesema alikamatwa pamoja na rafiki zake baada ya polisi kuwakuta na silaha butu pamoja na bangi, jambo ambalo amedai liliwapelekea kufunguliwa mashtaka na kuwekwa korokoroni.
Rudra Kartel ambaye amekiri kuwa alikuwa anafanya biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya amesema aliachiwa huru juzi kati baada ya wazazi wake na wanafamilia kuchangisha ย ya shillingi elfu 150 kama dhamana ya kumtoa jela.
Hata hivyo amesema kwa sasa amekuwa mtu mwema huku akidokeza kuwa ameanza shughuli zake za kimuziki chini ya uongozi wa 32 Empire.
Utakumbuka Rudra Kartel alipata umaarufu nchini ย baada ya staa wa dunia Vybz Kartel kumposti kupitia ukurasa wake Instagram lakini pia akiwa chini Magix Empire ambayo ilikuwa inamilikiwa na prodyuza Magix Enga ila alijiondoa baadae kufuatia ugomvi ulioibuka kati yao.