DIAMOND PLATINUMZ APEWA JEZI NA TIMU KUBWA USA

DIAMOND PLATINUMZ APEWA JEZI NA TIMU KUBWA USA

Msanii mwenye tuzo nyingi zaidi Afrika Mashariki na Kati Diamond Platnumz amepewa heshima kubwa na timu ya Mpira wa Marekani inayofahamika kama washington NFL. Diamond amekabidhiwa jezi namba 99 huku ikipambwa na jina lake mgongoni Platnumz. Timu hiyo ambayo inashikilia nafasi ya pili kwenye Ligi ya mpira wa Marekani imechapisha picha hizo za Diamond kwenye ukurasa wao wa Instagram na kuandika “diamond platnumz repping the Burgundy & Gold” Diamond Platnumz anakuwa msanii wa pili kutoka bara la Afrika kukabidhiwa Jezi na timu kubwa za mpira duniani baada ya siku chache zilizopita burna boy kupewa jezi na klabu ya Manchester United Diamond kwa sasa yupo nchini Marekani kwaajili ya ziara ya kimuziki ambapo mpaka sasa ameshatumbuiza kwenye miji miwili.

Read More
 WILLY PAUL: SIHITAJI SUPPORT YA WASANII WA KENYA KWENYE THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

WILLY PAUL: SIHITAJI SUPPORT YA WASANII WA KENYA KWENYE THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

Hitmaker wa Lenga msanii Willy paul ametoa ya moyoni baaada ya baadhi ya wasanii nchini kuzuzia kumpa support kwenye album yake ijayo  iitwayo The African Experience. Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amewatolea uvivu wasanii ambao amewataja kama wanafiki kwa kusema kwamba ahitaji watu wa sampuli hiyo kumuunga mkono wakati huu anajianda kuiachia album yake mpya. Bosi huyo wa Saldido ameenda mbali zaidi na kusema kwamba alizaliwa na atakufa pekee yake hivyo haitaji support ya mtu yeyote kwani Mungu yupo upande wake. The Africa Experience album kutoka kwa mtu mzima Willy paul inatarajiwa kuingia sokoni rasmi Oktoba 24 mwaka ingawa hajatuambia  idadi ya nyimbo ambazo zitapstikana kwenye album hiyo. Hii itakuwa ni Album yake ya pili, baada kuachia  album yake ya kwanza mwaka wa 2020 iitwayo songs of solomon ikiwa na jumla ya mikwaju kumi ya moto.

Read More
 HITMAKER WA “MAPEPO” VISITA AFILISIKA KIUCHUMI, AOMBA MSAADA KWA WAHISANI.

HITMAKER WA “MAPEPO” VISITA AFILISIKA KIUCHUMI, AOMBA MSAADA KWA WAHISANI.

Msanii tajika nchini Visita ametoa wito kwa wahisani kumsaidia kifedha kwani amefilisika kiuchumi na hana mahala pakuishi. Akiwa kwenye moja ya interview visita amesema kwa sasa anaishi kwenye studio ya kurekodia muziki inayomilikiwa na rafiki yake mmoja. Hitmaker huyo wa Mapepo amesema alifurushwa kwenye  nyumba aliyokuwa akiishi kutokana na malimbikizi ya kodi aliyokuwa akidaiwa. Mwezi Mei mwaka huu rapa huyo alichangiwa pesa na wasanii wenzake pamoja na marafiki mara  baada ya kushindwa kulipa gharama ya matibabu alipokuwa amelezwa hospitalini. Visita ni moja kati ya wasanii walioacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini na anafahamika na hits kama Mapepo,Dawa ya moto, Dumbala Remix, Hivo ndio Kunaendanga, Fimbo na nyingine kibao. Ikumbukwe tangu ujio wa msala wa corona wasanii wengi  nchini wameathirika kiuchumi na kimawazo baada ya kufungiwa matamasha ya muziki ambayo wamekuwa wakitegemea kuchuma riziki.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANI KEYSHIA COLE.

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MWANAMUZIKI KUTOKA MAREKANI KEYSHIA COLE.

Siku kama ya leo oktoba 15 mwaka wa 1981 alizaliwa staa wa muziki wa RnB kutoka marekani Keyshia Cole. Jina lake halisi ni Keyshia Myeshia Johson na alizaliwa huko Oakland Carlifonia nchini Marekani ambako alianza kujifunza kuimba ambapo marafiki zake walimtambulisha kwa rap mkongwe nchini marekani MC Hammer akiwa na miaka 12 tu na kutaka kuimba naye. Keyshia baadae alijenga urafiki na 2 Pac ambaye alimwambia atamsaidia kwenye kumjenga kimuziki lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kufanya kazi na rapa huyo ambaye alikuja akafariki baada kupigwa risasi. Akiwa na miaka 18 Keyshia Cole alihamia mjini Los Angeles  na kuanza kufanya kazi na wasanii kama D’Wayne Wiggings  wa  Tony Toni Tone na Messy Marv. Mwaka 2002, alitambulishwa kama msaani wa lebo ya muziki ya A&M Records A&R Ron baada ya boss wa lebel hio kusikia wimbo wake wa “Love” ukiwa bado hujakamilika ila ulivyokamilika ulikuwa wimbo wa kwanza wa Keyshia Cole kuuza kopi milioni 1 nchini Marekani. Mwaka wa 2005 Keyshia Cole aliachia album yake ya kwanza iitwayo The Way It Is  album ambayo ilifanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya gold na platinum kwa kuuza zaidi ya nakala milllioni 1.6. Baada ya kuachana lebo ya muziki ya A& M record alijiunga na lebo ya Geffen Records ambayo ilisimamia kazi zote za album yake ya pili   iliyotoka mwaka 2007 inayokwenda kwa jina la Just Like You. Album hiyo ilifanikiwa kupata mapokezi mazuri nchini marekani kwani ilifanikiwa kushika namba 2 kwenye chati ya Billboard 200 lakini pia iliweza kufikia viwango vya mauzo ya platinum kwa kuuza zaidi ya nakala milllioni 1.7 nchini marekani pekee. Mpaka sasa KeyshiaCcole ameshafanya jumla ya album saba za muziki, single 17, soundtrack album 6, na ameshirikishwa na wengine kwenye album 18 za muziki.

Read More
 TYGA AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUMPIGA EX GIRLFRIEND WAKE

TYGA AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUMPIGA EX GIRLFRIEND WAKE

Staa wa muziki kutoka marekani Tyga amefunguliwa mashtaka kwa kumpiga mpenzi wake wa zamani Camaryn Swanson. Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, mrembo huyo alifika nyumbani kwa Tyga mishale ya saa 9 usiku Jumatatu wiki ambapo awali aliambiwa asifike nyumbani hapo. Taarifa zinaeleza kwamba Camaryn alikuwa amelewa, lakini Tyga alimruhusu aingie ndani kwa ajili ya kuzungumza naye. Baadaye zilianza kusikika kelele za Camaryn ambaye ameiambia polisi kwamba Tyga alikuwa akimrushia ngumi wakati wa majibizano yao. Mama yake mzazi alifika na kumchukua kisha kuwapigia simu polisi kutoa taarifa. Polisi walifika nyumbani kwa Tyga siku hiyo hiyo kwa ajili ya uchunguzi na Tyga ameripotiwa kuandikisha kutoa maelezo kwa upande wake ikiwa tayari amefunguliwa kesi ya unyanyasaji wa nyumbani. Camaryn ame-share picha zake za majeraha baada ya tukio hilo.

Read More
 ARSENE WENGER ASEMA KUNA UWEZEKANO WA OFFSIDE KUAMULIWA NA TEKNOLOJIA MWAKA 2022

ARSENE WENGER ASEMA KUNA UWEZEKANO WA OFFSIDE KUAMULIWA NA TEKNOLOJIA MWAKA 2022

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba maamuzi ya ‘Offside’ yakaamuliwa moja kwa moja kwa kutumia Teknolojia kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazofanyika nchini Qatar. Wenger ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maendeleo ya mpira wa miguu katika Shirikisho la Soka duniani FIFA, amesema hiyo itakuwa hatua kubwa kwenye soka la dunia kwani pia itapunguza lawana nyingi kwa waamuzi. Kwa sasa teknolojia imechukua nafasi kubwa kwenye mpira kwani maaumizi mengi nyeti yanafanywa na VAR na Goal Line Technology.

Read More
 KENRAZY AACHIA RASMI SON OF GOD ALBUM

KENRAZY AACHIA RASMI SON OF GOD ALBUM

Mkali wa muziki nchini Kenrazy ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la Son of God. Son of God album imebeba jumla ya mikwaju 20 ya moto huku ikiwa na kolabo 7 pekee. Kenrazy amewashirikisha wasanii mbali mbali wa humu nchini kama Bigpin, Kaya,Visita, Sosuun, Civa Ramah K na Young haze. Album ya “Son of God” ni album ya tatu kwa mtu mzima kenrazy baada ya Ti-chi ya mwaka wa 2008 na Get it Right from Kenrazy ya mwaka wa 2011. Hata hivyo Album hiyo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya  kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile youtube, na Spotify

Read More
 CHAMA CHA UGANDA MUSICIANS FEDERATION CHAANZA ZOEZI LA KUWASAJILI WASANII

CHAMA CHA UGANDA MUSICIANS FEDERATION CHAANZA ZOEZI LA KUWASAJILI WASANII

Msanii nguli kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amezindua zoezi la kuwasajili wasanii ambao wanatamani kujiunga na chama chake cha Uganda Musicians Federation. Ni Zoezi ambalo litaandeshwa na timu ya wataalam wa masuala ya muziki nchini Uganda ambao watawachagua  wasanii kutoka maeneo mbali mbali nchini Uganda. Ikumbukwe chama cha Uganda Musician Federation lilizunduliwa na Mwanamuziki Jose Chameleone  mwezi juni mwaka huu. Lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho lilikuwa ni kuangazia maslahi ya wasanii nchini uganda ambao wamekuwa wakisuasua kimuziki. Chameleone aliweza kuwasajili wasanii kama Pallaso, Weasel, Feffe Buusi na wengine wengi. Chini ya mwongozo wake, walipata fursa ya kukutana na Jenerali Salim Saleh kutafuta msaada wa kifedha lakini wachache wao walipewa pesa taslimu. Wanamuziki waliokosa pesa hizo walihamua kumkimbia chameleone jambo lilomlazimu bosi huyo wa Leone island kuchukua mapumziko mafupi.

Read More
 SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

Kundi maarufu la muziki nchini, Sauti sol limepokea cheti cha utambuzi yaani (Certificate of Recognition) kutoka kwa waandaji wa tuzo za Grammy.   Cheti hicho ni maalum kwa ajili ya ushiriki wao kama watayarishaji kwenye album ya msanii Burna Boy kutoka Nigeria iitwayo “Twice As Tall” ambayo ilishinda tuzo ya Best Global Music Album kwenye tuzo za 63 za Grammy zilizofanyika mwezi wa tatu mwaka huu.   Sauti sol wameshiriki kwenye uandaaji wa wimbo namba 11 kutoka kwenye album ya “Twice As Tall” uitwao ‘Time Flies’.   Ikumbukwe, Sauti Sol kwa sasa wapo nchini Uingereza kwa ajili ya ziara yao ya kimuziki baada ya mapumziko ya takribani miaka miwili kutokana na janga la Corona.    

Read More
 DIAMOND AONYESHA SAA YAKE MPYA YA ROLEX YENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLIONI 2.8

DIAMOND AONYESHA SAA YAKE MPYA YA ROLEX YENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLIONI 2.8

Staa wa bongofleva Diamond Platnumz ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozitolea jasho. Mkali huyo wa Naanzaje ametumia kiasi cha dolla 25,000 ambazo ni zaidi ya shilling milioni 2.8  kwa pesa ya Kenya kununua saa mpya aina ya Rolex. Hii ni kwa mujibu wa risiti ya ununuzi wa saa hiyo ambayo aliishare kwenye insta story yake kwenye mtandao wa Instagram. Diamond Platnumz ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki, alitembelea duka maarufu la Watch Empire huko Los Angeles na kujipatia saa hiyo yenye warantii ya miaka miwili. Diamond anaungana na mastaa kama Davido, Drake, Jay Z, Kanye West  ambao hupendelea kuvaa saa za aina ya Rolex.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MKALI WA RnB KUTOKA MAREKANI USHER

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MKALI WA RnB KUTOKA MAREKANI USHER

Siku kama ya leo Oktoba 14 mwaka wa 1978 alizaliwa Staa wa muziki RnB kutoka nchini Marekani Usher. Jina lake halisi ni Usher Raymond IV na alizaliwa huko Dallas, Texas nchini na kukulia Atlanta, Georgia nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 1994 alipoachia album yake ya kwanza iitwayo Usher. Lakini mwaka wa 1997 ndipo Usher alipopata umaarufu baada ya kuichia albamu yake ya pili iitwayo MY WAY,ambayo ndani yake kulikuwa na wimbo uitwao NICE & SLOW ambao ulishika namba moja kwenye Billboard hot 100. Hakuishia hapo,albamu yake tatu ya mwaka wa 2001 iliyoitwa 8701 ilitoa wimbo ambao wengi leo tunaimfahamu kwa jina la U REMIND ME ambao nao ulishika namba moja pia kwenye Billboard hot 100. Mwaka 2004 alitoa albamu ya nne iliyoitwa CONFESSIONS albamu iliyouza zaidi  ya nakala million 10 kwa marekani pekee na kupewa hadhi ya viwango vya mauzo ya DIAMOND,ndani yake kulikuwa na vibao vikali kama YEAH,BURN na MY BOO. Mwaka 2008 usher alitoa albamu ya tano iitwyo HERE I STAND ndani kukiwa na hits kali kama LOVE IN THIS CLUB ambayo nayo ilishika namba moja kwenye chati ya Bllboard hot 100. Hata hivyo mpaka sasa usher ameshafanya jumla ya album 8 za muziki, EP 8, Singles 79 na album 10 za nyimbo zilizotoka pamoja na zile hazikutoka akiwa chini ya lebo ya muziki ya La Face,Arista, Jive na RCA Records. Kutokana na mafanikio ambayo aliyapata kwenye muziki wake nchini marekani Usher ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo mbali mbali za muziki na ameshinda tuzo 8 za Grammy, 18 za Billboard music Awards, 34 za ASCAP Awards, 9 za Soul train music na nyinngine kibao Kando na muziki, usher ni mmiliki wa record lebo iitwayo vanity records na pia ameigiza kwenye filamu mbali mbali nchini marekani ikiwemo the Faculty ya mwaka wa 1998, Light it up ya mwaka wa 1999, Hustlers ya mwaka wa 2019 miongoni mwa nyingine kibao.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 13, ALIZALIWA MKALI WA RnB NA HIPHOP KUTOKA MAREKANI ASHANTI

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 13, ALIZALIWA MKALI WA RnB NA HIPHOP KUTOKA MAREKANI ASHANTI

Siku kama ya leo Oktoba 13 mwaka wa 1980 alizaliwa staa wa muziki wa RnB na Hihop kutoka nchini Marekani Ashanti.   Jina lake halisi ni Ashanti Shequoiya Douglas na alizaliwa huko Glen Cove, New York nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 2001 kipaji chake kilipotambuliwa na prodyuza mkali kutoka marekan Irv Gotti ambaye alimshirikisha kwenye wimbo uitwao Whats Luv  wake Fat Joe na always on time wa Jah Rule.   Kutokana na uwezo ambao alionyesha kwenye collabo hizo Ashanti alisaini mkataba wa kufanya kazi na lebo ya muziki Murder Inc ambayo ilisimamia kazi zote za album yake ya kwanza iitwayo Eponymous ya mwaka wa 2002,album ambayo iliweza kufikia viwango vya mauzo ya Platinum kwa kuuza zaidi ya nakala milllioni 6 nchini Marekani.   Mwaka wa 2003 ashantia aliachia album yake ya pili iiitwayo Chapter II ambayo ilifanikiwa kushika namba moja kwenye chati ya billboard 200 lakini pia ikafanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya platinum kwa kuuza nakala millioni 1.5.   Mwaka huo huo Ashantia aliachia ya tatu iiitwayo Christmas ikafuatwa na Concrete Rose ya 2004, Declaration ya mwaka wa 2008 na Braveheart ya 2014 album ambazo hazikufanya vizuri kwenye soko la muziki ikilinganishwa na album zake za awali.   Hata hivyo mpaka sasa ashanti ameshafanya jumla album 6 za muziki, singles 24,  na video 21 za muziki wake akiwa chini lebo ya muziki  Murder Inc,Def Jam na Motown.   Kutokana na mafanikio ambayo aliyapata kwenye muziki wake nchini Marekani Ashanti ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo 89 za muziki na ameshinda tuzo 35 ikiwemo  8 za Billboard Music Awards, 3 za American Music,moja ya Grammy na nyinngine kibao.   Kando na muziki, Ashanti ni muigizaji ana ameshiriki kwenye filamu nyingini nchini marekani ikiwemo  Coach Carter,John  Tucker Must Die na nyingine kibao.

Read More