CHANNEL ZA R. KELLY YOUTUBE ZAFUNGIWA KUFUATIA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO.

CHANNEL ZA R. KELLY YOUTUBE ZAFUNGIWA KUFUATIA MASHTAKA YA UNYANYASAJI WA KINGONO.

Kufuatia mashtaka ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo na makosa mengine yanayomkabili nguli wa muziki wa R&B duniani, R. Kelly, mtandao wa Youtube umechukua hatua ya kuzifungia channel rasmi za staa huyo.   Channel hizo ni pamoja na R Kelly TV na R Kelly Vevo ila, nyimbo za nguli huyo bado zipo Youtube kupitia channel za watu wengine.   Kwa sasa R.Kelly anasubiria hukumu yake ambayo imetajwa kutolewa Mei 4 mwakani, na huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 au kifungo cha maisha gerezani.            

Read More
 DADDY ANDREA NA ANGELLA KATATUMBA WAFUFUA TENA PENZI LAO

DADDY ANDREA NA ANGELLA KATATUMBA WAFUFUA TENA PENZI LAO

Wasanii Angella Katatumba na Daddy Andrea walivunja uhusiano wao mwaka wa 2020 baada andrea kudinda kufanya vipimo vya HIV.   Kwenye mahojiano mbali mbali Daddy Andrea alithibitisha kwamba hajawahi mpenda Angella Katatumba na jambo hilo lilimsumbua sana mrembo huyo.   Andrea alienda mbali zaidi na kuanza mahusiano mapya na Nina Roz ila mahusiano yao yalikuja yakiingiwa na ukungu kwa madai ya usaliti na kumvunjiana heshima.   Sasa mapya yameibuka  baada ya Angella Katatumba kuthibitisha kwamba wamerudiana na Daddy Andrea kwenye moja ya interview.   Hitmaker huyo wa amesema amerudiana na mpenzi wake wa zamani Daddy Andrea baada ya prodyuza huyo kumuomba msamaha.   Wawili hao wamedai kwamba tayari wamerekodi wimbo wa pamoja uitwao Wendi ambao utatoka hivi karibuni.   Ikumbukwe daddy andrea na Angella Katatumba wapo chini ya lebo ya muziki ya black market records ambayo inasimamia kazi zao za muziki.    

Read More
 RHINO KING WA THE MAFIK AWEKA WAZI KUHUSU HATMA YA KUNDI HILO

RHINO KING WA THE MAFIK AWEKA WAZI KUHUSU HATMA YA KUNDI HILO

Msanii aliyekuwa akiunda kundi la the Mafik, Rhino ameweka wazi juu ya hatma ya kundi hilo kufanya kazi kwa pamoja kama ilivyokua awali.   Akitumia ukurasa wake wa Instagram kujibu maswali ya mashabiki waliotaka kujua hatma ya kundi hilo lililofanya vizuri na wimbo wa passenger, rhino amejibu kua kundi hilo halipo tena wala halitakuja kuwepo tena.   Ikumbukwe kundi la the mafik lilikuwa linaundwa na wasanii Rhino, mbala mwezi na Hamadai lakini tangu msanii mbala mwezi Afariki mwaka wa 2019 kundi hilo limekuwa likisuasua kimuziki.          

Read More
 INSTAGRAM YAONDOA IGTV

INSTAGRAM YAONDOA IGTV

Mtandao wa Instagram umetangaza kuunganisha IGTV (video ndefu) na video za Feeds (video za posts za kawaida) ambapo zote zitaitwa Instagram Video.   Instagram imeondoa jina la IGTV na video ndefu zitabaki kama kawaida lakini hazitaitwa IGTV. Video za feeds ambazo huwa na urefu wa sekunde 60, zote zitaitwa Instagram Video huku Reels zikibaki kuwa video fupi ambazo zitakuwa na style ya video za TikTok.   Katika profile za watumiaji wa Instagram, itabaki tab ya Feeds ambayo itakuwa na posts za picha, Reels, na Instagram Videos na app ya IGTV itaitwa Instagram TV.            

Read More
 WHATSAPP MBIONI KUJA NA UWEZO WA KUENDELEA KUSIKILIZA VOICE MESSAGES HATA UKIWA UMEFUNGA CHATS

WHATSAPP MBIONI KUJA NA UWEZO WA KUENDELEA KUSIKILIZA VOICE MESSAGES HATA UKIWA UMEFUNGA CHATS

App ya WhatsApp inafanya majaribio ya kuweka mfumo mpya wa “Voice Message au Notes”. Mfumo huo mpya utawezesha watumiaji kuendelea kusikiliza Voice Message hata ukiwa umefunga chat na kufungua chat nyingine au kurudi kwenye list ya messages.   Kwa kawaida ukiwa unasikiliza Voice Message katika WhatsApp, ukiifunga chat na Voice Message inaacha kucheza, hivyo inabidi ubaki katika chat ikiwa unataka kusikiliza Voice Message. Mfumo mpya wa Voice Messages utawezesha mtumiaji kuendelea kusikiliza Voice Message huku akiwa amefungua chat nyingine tofauti na chat ambayo Voice Message imetumwa.   Kwa juu itakwepo line ya rangi ambayo inafanana na Audio Player ambapo mtumiaji atakuwa na uwezo wa ku-pause, Play na kufunga Voice Message. Lakini pia  voice note hiyo itakuwa na uwezo wa kuonyesha jina na profile ya chat ambayo imetuma Voice Message.  Itasaidia endapo kama kuna chats nyingine ambazo inakubidi ufungue kwani utakuwa na uwezo wa kuendelea na shughuli nyingine katika app hiyo huku ukisikiliza Voice Message kwa pamoja.   Feature hii ipo katika majaribio katika mfumo wa iOS, na itatoka kabla ya mwaka huu kuisha. Ni mabadiliko ambayo tayari yapo Telegram kwa muda mrefu sana.            

Read More
 B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

Msanii wa muziki nchini Kenya, Dennis Manja maarufu kama B Classic ameachia wimbo wake wa mwisho baada ya kutangaza nia yake ya kutaka kuacha muziki.   B Classic alidai kuwa anaacha muziki na kugeukia kazi ya ufundi wa magari baada ya kutoridhishwa na mapokezi ya kazi zake pindi anapoachia muziki mpya.   B Classic mkali wa wimbo wa Pisi Kali uliofanya vizuri mapema mwezi Agosti mwaka huu, ameachia  ‘Utawezana Kweli’, wimbo anaodai kuwa itakuwa kazi yake ya mwisho.   Wimbo huo umetayarishwa na Prodyuza Denzel huku video ikaongozwa na Director Rahim chini ya lebo ya muziki ya Champions Studio yenye makao yake jijini Nairobi.            

Read More
 AFRO EAST ALBUM YA HARMONIZE YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 2.5 BOOMPLAY

AFRO EAST ALBUM YA HARMONIZE YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 2.5 BOOMPLAY

Album ya Mwanamuziki harmonize iliyotika Machi 14 mwaka wa 2020 Afro East yenye nyimbo 17 imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Million 2.5 katika mtandao wa boom play music.   Kwa upande wa Album, album yenye streams nyingi katika mtandao huo kwa wanamuziki wa tanzania ni album ya Mwanamuziki rayvanny Sound From Africa ambayo ina jumla ya streams millioni 15.5 katika mtandao huo maarufu wa kusimamia na kuuza kazi za muziki.   Sound From Africa album ya mtu mzima Rayvanny iliingia sokoni Rasmi februari mosi mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 23 ya moto            

Read More
 WIMBO WA C-KAY LOVE  NWANTITI WAONGOZA KWA STREAMS SPOTIFY

WIMBO WA C-KAY LOVE NWANTITI WAONGOZA KWA STREAMS SPOTIFY

Hitmaker wa ngoma ya Love Nwantiti C-kay ameendelea kufanya poa haswa upande wa streams katika mtandao mbalimbali ya kuuza na kusikiliza muziki duniani. Hii ni baada ya kufikisha zaidi ya wasikilizaji Million 17 ndani ya mwezi yaani monthly listeners katika mtandao wa Spotify. C-Kay anakuwa msanii wa kwanza kutoka barani Africa kufikisha jumla ya wasikilizaji hao millioni 17.4 ndani ya mwezi mmoja ,akiivunja rekodi ya mtu mzima burna boy mwenye wasikilizaji millioni 10.2 wa mwezi katika mtandao wa spotify.

Read More
 BRUNO K AMCHANA CINDY SANYU KWA KUSHINDWA KUWATETEA WASANII

BRUNO K AMCHANA CINDY SANYU KWA KUSHINDWA KUWATETEA WASANII

Mwanamuziki kutoka nchini uganda Bruno K amemtolea uvivu msanii mwenzake Cindy Sanyu hii ni baada ya msanii huyo kudai kwamba Bruno K alisaini mkataba na lebo ya muziki ya Black markert Records bila kuelewa mkataba wenyewe.   Akiwa kwenye moja ya interview Bruno K amesema madai ya Cindy ambaye ni rais wa chama cha wanamuziki nchini Uganda hayana msingi wote wote kwani kauli yake hiyo inaonyesha ni jinsi gani ameshindwa kuwatetea wasanii wanaonyanyaswa na lebo za muziki.   Bruno K kwa sasa anaendelea kushinikiza lebo ya muziki ya Black Market records impe channel yake ya youtube baada ya lebo hiyo kuchukua akaunti yake hiyo alipoigura lebo ya muziki ya Black Market  records.   Ikumbukwe juzi kati Cindy Sanyu aliwataka wasanii nchini uganda kuwa makini wanapotia sahihi mikataba na lebo za muziki kwani wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo bila kuwashirikisha mawakili.            

Read More
 RINGTONE APEWA NOTISI YA SIKU 10 KUONDOKA KWENYE NYUMBA YAKE YA RUNDA

RINGTONE APEWA NOTISI YA SIKU 10 KUONDOKA KWENYE NYUMBA YAKE YA RUNDA

Mwànamziki wa nyimbo za injili nchini Ringtone Apoko amepewa makataa ya siku kumi kuondoka kwenye nyumba anayoishi mitaa ya Runda jijini Nairobi.   Kulingana na barua ya kampuni ya mawakili ya AGN Kamau Advocates,  nyumba ambayo ringtone anaishi ni ya raia wa Sweden kwa jina Mona Ingegard aliyefariki mwaka wa 2007 na Ringtone alinunua nyumba hiyo bila kufuata njia sahihi.   Hata hivyo Ringtone ambaye amekuwa akijinadi kwamba ni mwanamuziki utajiri afrika mashariki hajatoa tamko lolote kuhusiana madai yaliyoibuliwa na kampuni ya wanasheria ya AGN Kamau Advocates.    

Read More
 MADINI CLASSIC ATANGAZA KUHAMIA KWENYE MAPENZI YA JINSIA MOJA

MADINI CLASSIC ATANGAZA KUHAMIA KWENYE MAPENZI YA JINSIA MOJA

Mkali wa muziki nchini Madini Classic amewashangaza wadau wa muziki nchini baada ya kutangaza kwamba amekukumbatia mapenzi ya jinsia moja kwani amechoshwa na mapenzi kabisa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha akiwa amejipodoa wanja, na lipstick kama mwanamke na kusema kwamba ameamua kuhamia mapenzi ya jinsia moja kwani siyo dhambi. Hitmaker huyo wa Toto la Kanairo amewaomba mashabiki wake kutomchukulia vibaya kwani ameumizwa sana kwenye mahusiano yake ya zamani hadi amekata tamaa kuanza mahusiano na wanawake. Hata hivyo mashabiki zake wameonekana kukerwa na kauli ya Madini Classic huku wengi wakimtaka atoe muziki mzuri badala ya kujihusisha na kiki zisizokuwa na msingi aachane na masuala ya kiki nmuziki kama ameshindwa kuipambania kazi

Read More
 VIDEO ZA OTILE BROWN ZAONDOLEWA YOUTUBE

VIDEO ZA OTILE BROWN ZAONDOLEWA YOUTUBE

Music Video za Staa wa muziki nchini otile brown zimeondolewa kwenye akaunti ya mtandao wa YouTube ya msanii huyo   Ukitembelea kwenye akaunti ya YouTube ya Otile Brown hutafanikiwa kuziona video za nyimbo kama Dusuma, Such Kinda Love, Chaguo La Moyo Wangu na Aiyana kutokana na kuondolewa na aliyezi-upload   Mpaka sasa haijafahamika sababu za kushushwa kwa video hizo za Otile Brown.   Chaguo la Moyo wangu na Dusuma ni video za muziki zenye watazamaji wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Kenya            

Read More