Gossip

Bahati Asema Ana Fedha za Kutosha Kukaa Mwaka Mzima Bila Kufanya Kazi

Bahati Asema Ana Fedha za Kutosha Kukaa Mwaka Mzima Bila Kufanya Kazi

Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Bahati, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kudai kuwa ana fedha za kutosha kumwezesha kukaa bila kufanya kazi kwa kipindi chote cha mwaka 2026.

Kupitia mitandao ya kijamii, Bahati amejigamba kuwa ana fedha za kutosha na kuambatanisha kauli hiyo na kuonesha magari yake ya kifahari aina ya Mercedes-Benz G-Wagon pamoja na Range Rover, huku akisisitiza kuwa mafanikio yake ya kifedha yanamruhusu kuchukua mapumziko marefu bila kuathiri maisha yake.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya msanii huyo kushambuliwa vikali na baadhi ya Wakenya mtandaoni, kufuatia madai yake kuwa yeye ndiye msanii pekee mwenye mafanikio makubwa kuwahi kutokea nchini Kenya.

Kauli hiyo iliwakera wengi waliodai kuwa ni ya kujikweza na kuwadharau wasanii wengine waliotoa mchango mkubwa katika tasnia ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *