Msanii nyota wa Bongo Fleva Zuchu amezua mjadala mitandaoni baada ya kuonekana akimzuia shabiki wa kike aliyekuwa akitaka kumkumbatia mume wake, Diamond Platnumz, wakati akiwa location kwenye video shoot ya wimbo wao uitwao Inama.
Kwa mujibu wa video inayosambaa mitandaoni, Zuchu alionekana awali akizungumza na shabiki huyo kwa utulivu. Hata hivyo, hali ilibadilika pale shabiki huyo alipojaribu kuelekea eneo alilokuwepo Diamond. Zuchu alichukua hatua ya haraka na kumzuia, akionesha wazi kutoridhishwa kwake na jaribio hilo.
Katika video hiyo, Hitmaker huyo wa Amanda amesikika akiwaagiza mashabiki kumsalimia Diamond kwa mikono, kitendo ambacho wengi wametafsiri kama dalili ya wivu wa kimapenzi, wakieleza kuwa huenda Zuchu alikuwa akilinda mipaka ya ndoa yake.