Mtangazaji na mdau wa burudani kutoka Tanzania, Mwijaku, amefunguka mpango wa kukodisha nyumba yake ya billioni 1.3 kutokana na kupitia kipindi kigumu cha upweke baada ya mke wake kumkimbia.
Kupitia ukurasa wake wa Insta, Mwijaku amesema anafikiria kupangisha jumba hilo ili kubadilisha mazingira na kupunguza mawazo makali yanayomkabili. Amesema nyumba hiyo kubwa aliyokuwa akiitamani kwa miaka mingi kwa sasa imepoteza maana, akifananisha hali yake na kuishi kwenye kaburi kutokana na kukosa watu wa karibu wa kushiriki nao maisha.
Mwijaku amesisitiza kuwa tukio la mke wake kumkimbia limemfundisha somo kubwa maishani, akibainisha kuwa nyumba au mali hazina thamani bila uwepo wa familia na watu wanaokupa furaha.
Hata hivyo amewashauri watu kutokupima furaha kwa fedha au mali pekee, akisisitiza kuwa amani ya moyo, familia na upendo ndio msingi wa furaha ya kweli duniani.