
Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana Marua amepata pigo kubwa baada ya kupoteza chaneli yake ya YouTube kwa wadukuzi.
Diana Marua ametumia ukurasa wake wa Instagram, kutangaza taarifa hiyo mbaya kwa mashabiki zake ambayo imemuacha akikadiria hasara. Akaunti hiyo yya youtube ambayo ilidukuliwa ilikuwa na zaidi ya subscribers laki 6 tangu ajiunge na mtandao huo Agosti 19 mwaka wa 2019.
Marua mwenye uhuzuni amesema kwamba wadukuzi walianza kwa kubadilisha jina lake la Yoiutube kabla ya kuifuta akaunti yake hiyo.
“😭😭😭😭😭😭😭😭 Nimeishi kwa amani na kila mtu na siku zote nimekaa kwenye njia yangu; Sijui kwanini mtu yeyote angenifanyia hivi! Unadukua akaunti yangu ya YouTube; badilisha jina na mbaya zaidi unaifuta 😭😭😭😭😭😭😭😭,” alisema.
Hata hivyo, mwimbaji huyo wa One Day amewahakikishia mashabiki wake kwamba suala hilo linashughulikiwa na usimamizi wake na ana matumaini kwamba mambo yatarejea kama kawaida.
Katika ukaguzi uliofanywa na mwandishi huyu hukupa ujumbe unaosomeka: “Video haipatikani. Video hii haipatikani tena kwa sababu akaunti ya YouTube inayohusishwa na video hii imesimamishwa.
Chaneli ya Marua ilidukuliwa wakati alikuwa miongoni mwa WanaYouTube mashuhuri nchini Kenya ikizingatiwa kuwa amekuwaa akipata idadi kubwa ya watazamaji kila wakati anapopakia maudhui kwenye akaunti yake ya youtube..