Entertainment

Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Mtayarishi mkongwe wa muziki nchini Marekani Dr. Dre, amefunguka sababu za kuchagua upande kwenye bifu ya Drake na Kendrick Lamar iliyotikisa ulimwengu wa muziki wa Hiphop duniani. Akizungumza kwenye podcast ya The Unusual Suspects With Kenya Barris and Malcolm Gladwell, Dr. Dre ameeleza kuwa hakuvutiwa na hatua ya Drake kumshambulia Kendrick Lamar pamoja na familia yake.

“Ninapenda wimbo wa  ‘Not Like Us’. Lakini niliposikia Drake akisema mambo mabaya kuhusu mke wa Kendrick na watoto wake, nikasema ‘Ah, adios!’”, Alisema Dre.

Kauli ya Dr. Dre inakuja muda mfupi baada ya Drake kufungua kesi dhidi ya Universal Music Group kuhusu wimbo ‘Not Like Us’, ambao una mashambulizi makali dhidi yake.

Hii si mara ya kwanza Dre kuzungumzia ‘Not Like Us’. Novemba mwaka jana, aliusifu wimbo huo kwa kusema kuwa umeleta mshikamano mkubwa kwa muziki wa Hiphop nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *