LifeStyle

Dr. Ofweneke Ataka Pastor Kanyari na Tash Kumlinda Sky Dhidi ya Mitandao

Dr. Ofweneke Ataka Pastor Kanyari na Tash Kumlinda Sky Dhidi ya Mitandao

Mwanahabari na msanii wa vichekesho, Dr. Ofweneke, ametoa wito kwa Pastor Kanyari na Tash kumlinda binti yao Sky dhidi ya shinikizo la mitandao ya kijamii

Ofweneke amependekeza simu ya Sky ichukuliwe kwa muda ili kumpa nafasi ya kupona na kupata mwongozo sahihi bila shinikizo la umma.

Amesisitiza kuwa kipindi hiki kinapaswa kutumika kumsaidia Sky kupitia huzuni ya kumpoteza mama yake, Betty Bayo, kwa njia ya faragha na utulivu.

Kulingana na Ofweneke, malezi ya karibu na usaidizi wa kifamilia ni nguzo muhimu kwa mtoto anayepitia changamoto za kisaikolojia na kihisia baada ya msiba.

Dr. Ofweneke ameeleza kuwa mitandao ya kijamii mara nyingi huongeza presha kwa watoto na vijana, na hivyo ni busara kumlinda Sky dhidi ya maoni na shinikizo la umma wakati huu napitia kipindi kigumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *