LifeStyle

VJ Patelo Ataka Vijana Kuchukua Tahadhari Baada ya Kuongezeka kwa HIV

VJ Patelo Ataka Vijana Kuchukua Tahadhari Baada ya Kuongezeka kwa HIV

Msanii wa arbantone, VJ Patelo, ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kutoa kauli tata kuhusiana na taarifa za kuongezeka kwa maambukizi mapya ya virusi vya HIV nchini Kenya.

Kupitia video aliyochapisha kwenye mtandao wa TikTok, Patelo amesema kuwa takwimu hizo zinamfanya ajisikie vizuri kwa sababu zinatoa onyo kali kwa watu wanaofanya ngono kiholela.

Patelo amesisitiza kuwa wale wanaopenda kujihusisha na ngono kupita kiasi wanapaswa kutambua madhara ya tabia hizo. Kwa mujibu wake, ongezeko la maambukizi ni ujumbe mzito unaopaswa kuchukuliwa kwa umakini na jamii nzima ili kuongeza tahadhari na kuimarisha nidhamu.

Kauli hiyo imeibuka muda mfupi baada ya Ripoti ya Makadirio ya HIV 2025 iliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa ya Mlipuko (NSDCC) kuonyesha kuwa Kenya imerekodi maambukizi mapya 19,991, ikilinganishwa na 16,752 mwaka uliopita.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa maambukizi mapya yanajitokeza zaidi miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 34, huku kaunti kumi zikichangia jumla ya asilimia 60 ya visa vipya. Kaunti hizo ni pamoja na Nairobi, Migori, Kisumu, Homa Bay, Busia, Siaya, Kakamega, Nakuru, Mombasa, na Bungoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *