Entertainment

Dyana Cods Ajivika Taji la Mwandishi Bora wa Nyimbo Nchini Kenya

Dyana Cods Ajivika Taji la Mwandishi Bora wa Nyimbo Nchini Kenya

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Dyana Cods, amezua taharuki kwenye tasnia ya burudani baada ya kujitangaza hadharani kuwa yeye ndiye mwanamke pekee mwenye uwezo mkubwa zaidi wa uandishi nyimbo nchini humo.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, msanii huyo amejipa taji la “Best Female Lyricist in Kenya” huku akiwapa changamoto wasanii wenzake wa kike kwa kuwataka mashabiki kuwataja au ‘kuwatag’ rappers au waimbaji ambao wanafikiri wanaweza kumshinda kwa ufundi wa kupanga maneno.

Kauli hiyo imetafsiriwa na wengi kama dharau kwa wakali wengine wa kike kwenye muziki huku kukiwa na msisimko wa kutaka kuona kama kuna msanii yeyote atakayejitokeza kupokea changamoto hiyo na kuchuana naye kwenye ulingo wa uandishi wa mashairi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *