Entertainment

Toxic Lyrikali Atangaza Ujio wa Show yake Qatar

Toxic Lyrikali Atangaza Ujio wa Show yake Qatar

Msanii wa rap kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, ametangaza rasmi onesho lake la kwanza la kimataifa litakalofanyika jijini Doha, nchini Qatar tarehe 9 Aprili katika ukumbi wa Avenue X Lounge.

Kupitia kurasa zake za kijamii, Toxic Lyrikali amesema kuwa onesho hilo la Doha ni hatua kubwa katika safari yake ya muziki, akiahidi kuwapa mashabiki wake wa ughaibuni burudani kali

Rapa huyo, amesema kuwa licha ya changamoto na mijadala inayoendelea mtandaoni kuhusu muziki wake, ataendelea kusonga mbele na kupanua mipaka ya kazi yake kimataifa bila uwoga wowote.

Hii itakuwa mara yake ya kwanza kwa Toxic Lyrikali kutumbuiza nje ya Kenya, hatua inayotafsiriwa kama kupanuka kwa wigo wa muziki wake kimataifa.

Ikumbukwe tangazo hilo limekuja siku chache tu baada ya msanii huyo kugonga vichwa vya habari kufuatia bifu yake na kundi la Buruklyn Boyz ambapo kila upande umekuwa ukiachia mfululizo wa diss tracks ukionyesha kujiamini katika ubora wao wa kazi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *