Gossip

Eric Omondi Aanza Harakati za Kumtafuta Jamaa Anayefanana Naye

Eric Omondi Aanza Harakati za Kumtafuta Jamaa Anayefanana Naye

Mchekeshaji na mwanaharakati, Eric Omondi, ameomba msaada wa kumtafuta kijana anayefanana naye, ambaye video yake imesambaa mtandaoni nchini Kenya.

Kupitia kipande cha video alichopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Eric ameeleza kuwa anataka kumpata kijana huyo ili wawe wawili, akitania kwamba mmoja wao anaweza kushiriki kwenye maandamano huku mwingine akiendelea na kazi zake za kawaida.

Kijana huyo ambaye anadaiwa kutoka Githurai, Kenya, alipata umaarufu ghafla baada ya video yake kusambaa ambapo alinukuliwa akisema kuwa anatamani kukutana na Eric Omondi. Wafuasi wengi mitandaoni wamekuwa wakimtag Eric kwenye video hiyo wakimtaka atimize ombi hilo.

Hadi sasa Eric Omondi hajaweka wazi kama amepata mawasiliano ya kijana huyo, lakini mashabiki wanatarajia kuona mkutano wao, ambao wengi wanaamini utazua kicheko na kufunika mitandao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *